23 Septemba 2024 - 17:52
Maimamu Watoharifu (a.s) ni Maasumina (hawana Uchafu wa dhambi na maasi) na Wafuasi wao wanapaswa pia kujitahidi katika kujiepusha na dhambi na maasi

Mmoja wa Marajii wa ngazi za juu wa Shia Ithna Ashari amesema: Hawzat na Chuo Kikuu huhuisha Jamii na Jufunga njia ya upotofu, ili watu wafuate njia ya Maimamu (Wasafi na Waliotakasika kutokana na madhambi), ili nao wawe wasafi (na waliotakasika kutokana na madhambi).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Sherehe ya kuvishwa kilemba kundi la Wanafunzi ilifanyika kupitia Ayatollah al-Udhma Jawad A'mouli sambamba na Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mkarimu wa Uislamu (Rehema na Amani ziwe iwe juu yake na Aali zake), na kuzikwa kwa Imam Jafar Sadiq (Amani iwe juu yake).

Katika sherehe hizo, Ayatollah Javadi A'mouli akiwatakia baraka na kuwapongeza Waumini kwa Mnasaba wa Siku hizi amesema:

Imamu Sadiq (amani iwe juu yake) aliitwa Jina hilo kupitia Mtume Muhammad (s.a.w.w) kabla hajazaliwa ambapo alisema(s.a.w.w):

"Mtoto wa sita wa familia hii ni Jafar Sadiq".

Akasema: Mwanadamu anatazamia (anasaka daima) uzima wa milele na maji ya uzima, na hii ni tamaa nzuri (au ni kutamani kuzuri), lakini ni lazima tujue kwamba 'maji haya ya uzima' na 'maji ya maisha' sio kama yale maji ya mvua inayonyesha kutoka mbinguni, na wala sio kama yale maji ya chemchemi yanayochimbuka na kumiminika toka ardhini, bali ni kama vile Mwenyezi Mungu anavyosema ndani ya Qur'an Tukufu:

 ﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ ﴾

"Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele".

[ Surat Al-Anfal: Aya ya 24]

_

Kisha akasema: Ikiwa mtu anataka kuishi maisha ya ukamilifu na ya uadilifu, na kama anataka kuishi kama Malaika, basi ni lazima amtii Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (s.a.w.w).

Katika sehemu nyingine ya hotuba ya Ayatollah Jawad A'mouli, anasema:

Baadhi ya watu wanajisahau kwamba ni wapi walikotoka, na kwa nini walikuja!.

Inatakiwa ichunguzwe ni nini chanzo cha usahaulifu huu. Jinai hizi zinazofanywa na Wazayuni na Wamagharibi dhidi ya Taifa la Palestina, ni kwa sababu hao wamejisahau, Mwenyezi Mungu anasema:

﴿وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ نَسُوا اللَّهَ فَأَنْسَاهُمْ أَنْفُسَهُمْ﴾

"Wala msiwe kama wale walio msahau Mwenyezi Mungu, na Yeye akawasahaulisha nafsi zao.

[Suratul - Hashr: Aya ya 19].

 _

Siri ni kwamba Mwanadamu anajisahau nafsi yake kwa sababu hakumbuki Tauhidi (Kumpwekesha Mwenyezi Mungu), wanaomsahau Mwenyezi Mungu wamejisahau wenyewe nafsi zao! Watu kama hao wanajali (wanafikra) Dunia tu!

Hadithi Tukufu isemayo:

 "Atakaye jifahamu nafsi yake, atakuwa amemfahamu Mola wake"

Ipo mkabala na Aya hiyo ya Qur'an Tukufu, kwa maana kwamba:

Hadithi hii na Aya hiyo ya Qur'an Tukufu, zina maelewano na Mashirikiano ya Kisayansi (Kiilmu), hapo katika Aya hiyo inasemwa kuwa:

"Usimsahau Mwenyezi Mungu, maana utajisahau mwenyewe nafsi yako"

Na hapa katika Hadithi hii inasemwa kuwa:

“Mtu yeyote atakaye jifahamu nafsi yake, atakuwa amemfahamu Mola wake”.

Hivyo, ikiwa (viwili hivi) Qur'an Tukufu na Ahlul-Bayt wa Isma na Utoharifu tutaviweka kando; basi kwa hakika Vita vya Kwanza na vya Pili vya Dunia, na jinai hii inayoendelea ndani ya Palestina na Gaza, (vyote hivyo) vitakuja.

Alieleza kuwa jambo pekee linalompa Mwanadamu "Uhai na Uzima wa Milele" ni "Dini ya Mwenyezi Mungu"

Alisema: Kwa mujibu wa Aya ya Utakaso, Ahlul-Bayt, Itrah wa Mtume (s.a.w.w) ni wasafi na wametakasika.

Qur'an Tukufu inasema katika Aya hiyo ya Utakaso:

﴿اِنَّما یُرِیدُ اللَّهُ لِیُذْهِبَ عَنْکُمُ الرِّجْسَ اَهْلَ الْبَیْتِ وَ یُطَهِّرَکُمْ تَطْهِیراً﴾

"Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul Bayt na anataka kukutakaseni utakaso ulio bora kabisa".

 [Suratul Ahzab: Aya ya 33].

_

Ikiwa Maimamu hao ni watakatifu na wasafi (kutokana na kila aina ya Video uchafu wa dhambi na maasi), basi kwa hakika Wanafunzi na Wafuasi wao pia wanapaswa kujaribu kuepuka dhambi na maasi.

Aalisema kuwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) alipojenga Msikiti wa Quba, iliteremshwa Aya isemayo:

  ﴿فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَنْ يَتَطَهَّرُوا﴾

"Humo wamo watu wanao penda kujitakasa"

[Surah At-Tawbah: Aya ya 108]

_

Maana yake ni kwamba:

Mpango (au Utaratibu) wa Msikiti ni mtu kuwa msafi / mtakatifu; Mtu wa Msikiti (ambaye Maisha yake yote ni Msikiti) anatakiwa kuwa msafi, mtu asokuwa huru, na anayefuata matamanio ya Nafsi yake, huyo sio msafi (sio mtakatifu).

Msikiti upo ili Mwanadamu awe huru. Msikiti sio tu kwamba upo ili Mwanadamu asiingie motoni, wapo wengi sana ambao hawaendi (hawataingia) motoni, bali Msikiti upo pia ili kutufundisha usafi (wa kujitoharisha na kujitakasa), na hilo liko juu sana kuliko hilo la Mwanadamu kwenda Peponi!

Aliendelea kusema:

Tuwafanye Maimamu wa Utoharifu (Amani iwe juu yao) kuwa mfano bora kwetu, ikiwa Itrah wa Mtume (s.a.w.w) ni Watoharifu, ikiwa Msikiti ni kwa ajili ya Utoharifu (na Utakaso), basi hilo lina maana kwamba Mtu wa Msikiti (yaani: Mtu yule anayelazimiana na kufungamana na Msikiti katika Maisha yake, huyo hakika) ni Mwanafunzi wa Ahlul-Bayt (a.s).

Nina matumaini kuwa Waislamu wote, Wana Hawzat wote, hasa nyinyi Wapendwa Wanafunzi, mtamkumbuka Mwenyezi Mungu ili msije kujisahau wenyewe nafsi zenu. Muwe Wanafunzi wazuri kwa Maimamu Watoharifu, na mziongoze jamii kuelekea kwenye usafi (utakasifu).

Ayatollah al-Udhma Jawad A'mouli alisema mwishoni wa Hotuba yake:

Mwenyezi Mungu amewataja Mashahidi katika Aya kadhaa za Qur'an Tukufu, kwamba Mashahidi wako hai, lakini hakuna mahali katika Qur'an Tukufu 'alipopia Mwenyezi Mungu kupitia Mashahidi', lakini Mwenyezi Mungu tunamuona akiapa katika Qur'an Tukufu kupitia "Kalamu na Wino wa Mwanachuoni", anasema:

 ﴿وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ﴾

"Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo!"

[Surat Al-Qalam: Aya ya 1]

Kwa nini Mwenyezi Mungu anaapa kwa Kalamu?!

Ni kwa kuwa hii ni Kalamu ya Aalim (Mwanachuoni) ambaye ni Shahidi, ni Hawzat na Chuo Kikuu ndio vinavyohuisha Jamii, ni Hawzat na Chuo Kikuu vinavyofunga njia ya upotofu ili watu wafuate njia ya Maimamu (wasafi na waliotakasika na dhambi) na ili wawe wasafi (waliotakasika na dhambi).